Elimu ya Afya

NINI NI KWELI NA NINI SI KWELI KUHUSU UGONJWA WA INI UNAOITWA HEPATITIS

Kuelekea Siku ya Ini Duniani, Tarehe 28/07/2023.
Tujifunze nini ni kweli ni nini si kweli kuhusu ugonjwa wa Ini unaoitwa “Hepatitis”

Si kweli: Hepatitis inaambukizwa kwa kujamiiana tu.

Kweli: inaambukizwa kwa kujamiiana bila kinga na mtu aliye na virusi,kupitia sindano zilizochafuliwa, kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua. Hepatitis A inaweza kuenea pia kupitia chakula na maji yaliyochafuliwa.

Si kweli 2: Hepatitis sio ugonjwa mbaya; ni maambukizi madogo tu.

Kweli: Hepatitis inaweza kutoka kuwa maambukizi mepesi ya muda mfupi hadi hali za kudumu kama vile Kansa ya ini na kuhatarisha maisha.

Si kweli 3: Hepatitis inaathiri tu watu wazee; vijana hawako hatarini.

Kweli: Mtu yoyote, bila kujali umri, anaweza kupata virusi.

Si kweli 4: Hepatitis haiwezi kuzuiwa; hakuna chanjo

Kweli: Kuna chanjo zinapatikana kwa hepatitis A na B. Chanjo hizi ni zenye ufanisi mkubwa katika kuzuia maambukizi

Hepatitis C mara nyingi inaweza kuponywa kwa dawa za kupambana na virusi ikiwa inagunduliwa mapema.

Karibu Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke kwa Ushauri, vipimo na Tiba.

read more
JE UNAJUA UKIPIGA MSWAKI HUTAKIWI KUSUKUTUA?

Je Unajua Ukipiga Mswaki Hutakiwi Kusukutua? Dr. Nasriya Ali, Anaelezea Jinsi ya Kupiga Mswaki Sahihi kwa Afya Bora ya Kinywa na Meno.*Unapofikiria kuhusu utunzaji wa afya ya kinywa, moja ya mazoea ya kila siku ambayo usipopiga kwa usahihi yanaweza kuathiri afya ya kinywa na meno .Lakini je, unajua kwamba kuna njia sahihi ya kufanya hivyo ili kuhakikisha afya bora ya kinywa na meno?

Kupiga mswaki ni hatua muhimu katika kudumisha afya ya kinywa na meno. Lakini mara nyingi, watu hufanya makosa yanayoweza kusababisha matatizo ya kinywa na meno. Dr. Nasriya Ali kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke anasema, "Moja ya makosa yanayofanyika ni suala la kusukutua baada ya kupiga mswaki. Kusukutua kunasababisha kuondoka kwa madini yaliyopo katika dawa ya mswaki ambayo yalitakiwa kubaki kwa ajili ya kulinda meno.

Dr. Nasriya Ali anashauri njia sahihi ya upigaji mswaki na vitu vya kuzingatia wakati wa kupiga mswaki. Hivyo basi Kabla hujaanza kupiga mswaki kuna vitu unatakiwa kuvizingatia

Tumia Mswaki mzuri

Mswaki mzuri ni ule wenye nyuzi au brashi laini, kulingana na umri wa mtumiaji. kuna miswaki ya watoto na ya watu wazima. Kutumia Mswaki wa aina hii utawezesha kufikia maeneo yote ya meno bila kusababisha madhara katika meno na fizi.

Kuzingatia aina ya dawa

unaweza kutumia dawa ya aina yoyote lakini dawa inapaswa kuwa na madini ya floride madini ya floride ni madini yanayozuia meno kutoboka na kufanya meno kuwa imara, na ndio maana unapo maliza kupiga mswaki hupaswi kusukutua na maji, unatakiwa kuacha hivyo hivyo ili kuruhusu madini yaliyopo katika dawa ya mswaki kufanya kazi yake katika kinywa chako.

Kupiga mswaki kwa usahihi au kutumia njia sahihi ya kupiga mswaki

njia sahihi ni kama ifuatavyo, utachukua mswaki wako na kuweka dawa ya meno yenye madini ya floride utaanza kupiga kwa taya moja moja kwa kupindisha mswaki wako kidogo kuelekea kulia ama kushoto, utaanza kupiga mswaki kwa mwendo wa kuzungusha taratibu ili kuwezesha mswaki kuingia katikati ya meno na kuepusha kuumiza fizi. Meno ya mbele juu unatakiwa kusimamisha mswaki na kusafisha. Utasafisha pia maeneo ya nyuma ya meno yanayohusika na utafunaji na utafanya hivyo hivyo kwa taya nyengine ni na kumalizia kwa kusugua ulimi kwa taratibu.

Muda unaotumia kupiga mswaki

Unatakiwa Kupiga mswaki kwa dakika zisizopungua dakika mbili, Unatakiwa kupiga mswaki mara mbili kwa siku yaani baada ya kunywa chai asubuhi ili kuzuia mabaki ya chakula yasiwepo kwenye kinywa muda mrefu na wakati wa kwenda kulala na kabla ya kulala unapaswa kupiga mswaki

Dr. Nasriya Ali anasisitiza umuhimu wa kutembelea daktari wa meno kwa ukaguzi na uchunguzi wa kawaida angalau mara mbili kwa mwaka. Anasema, "Uchunguzi wa kinywa na meno unaweza kugundua mapema matatizo yoyote na kuchukua hatua za haraka." Na katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke kuna madaktari bingwa na vifaa vinavyowezesha utoaji huduma sahihi wa kinywa na meno ambao watu wengi wanaweza wakapuuzia matatizo walionayo.

Kwa kumalizia, Dr.Nasria Ali anasema, "Upigaji mswaki ni mazoea rahisi lakini muhimu kwa afya ya kinywa na mwili kwa ujumla. Kwa kufuata njia sahihi na kujali afya yako ya kinywa, unaweza kuhakikisha una kinywa kizuri na chenye afya kwa maisha yako yote."
Kuwa na kinywa chenye afya ni muhimu sana kwa afya ya jumla. Kwa kuzingatia ushauri wa mtaalamu wa kinywa na meno, unaweza kuboresha afya yako ya kinywa na kufurahia maisha bora zaidi.

read more
FAHAMU KIPIMO HUSIKA CHA KUTAMBUA UGOJWA WA SIKO SELI (SICKLE CELL)

Selimundu/Siko seli

(Sickle cell) ni Ugonjwa wa kurithi, unaotokana na uwepo wa seli  za damu zenye umbo tofauti na la kawaida. Mtu mwenye tatizo hili huwa na changamoto ya kupungukiwa damu mara kwa mara , maumivu ya kichwa, viungo, pamoja na misuli.

Katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kupitia wizara ya Afya za kutoa elimu kwa Umma juu ya ugojwa wa siko seli (sickle cell) kutana na mtaalamu wa maabara Evelyne Mbaga kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke akielezea kipimo kinachopatikana hospitalini hapo chenye uwezo wa kutambua kama mtu anatatizo hilo la selimundu.

Kipimo hicho kwa lugha ya kitaalamu kinaitwa Hb Electrophoresis, kinatumika kuthibisha ugonjwa huo kwa kutoa asilimia ya kila aina ya hemoglobini ikiwemo hemoglobini ya selimundu

 Naye, Evelyne Mbaga ametoa ushauri kwa wana ndoa ambao wanatarajia kufunga ndoa, kuhakikisha wanafanya uchunguzi wa kutambua kama wana chembe chembe za selimundu zitakazo pelekea mtoto wao kuzaliwa na ugonjwa wa selimundu, kwani itarahisisha namna ya kumuangalia na kufuatilia afya yake.

read more
SIKO SELI(SICKLE CELL) NI NINI? JE UNAFAHAMU KIPIMO SAHIHI CHA SIKO SELI?

Selimundu(Sickle cell) ni Ugonjwa wa kurithi, unaotokana na uwepo wa seli  za damu zenye umbo tofauti na la kawaida. Mtu mwenye tatizo hili huwa na changamoto ya kupungukiwa damu mara kwa mara , maumivu ya kichwa, viungo, pamoja na misuli.

Katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kupitia wizara ya Afya za kutoa elimu kwa Umma juu ya ugojwa wa selimundu (sickle cell) kutana na mtaalamu wa maabara Evelyne Mbaga kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke akielezea kipimo kinachopatikana hospitalini hapo chenye uwezo wa kutambua kama mtu anatatizo hilo la selimundu.

Kipimo hicho kwa lugha ya kitaalamu kinaitwa Hb Electrophoresis, kinatumika kuthibisha ugonjwa huo kwa kutoa asilimia ya kila aina ya hemoglobini ikiwemo hemoglobini ya selimundu

Naye, Evelyne Mbaga ametoa ushauri kwa wana ndoa ambao wanatarajia kufunga ndoa, kuhakikisha wanafanya uchunguzi wa kutambua kama wana chembe chembe za selimundu zitakazo pelekea mtoto wao kuzaliwa na ugonjwa wa selimundu, kwani itarahisisha namna ya kumuangalia na kufuatilia afya yake.

read more