UVIMBE WA KILOGRAMU 15 WAONDOLEWA KATIKA KIZAZI CHA MWANAMKE ALIYEDUMU NAO KWA ZAIDI YA MIAKA 15
Posted on: June 18th, 2025
Mwananmke mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa amefanikiwa kufanyiwa upasuaji na Madaktari bingwa wa Upasuaji wakishirikiana na Mdaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake na Uzazi kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Temeke na kufanikiwa kuondoa uvimbe wenye uzito wa kilogramu 15 uliomsumbua kwa miaka 15
Upasuaji huo wa Kibingwa ulifanyika siku ya jumatau 16 Juni, 2025 chini ya jopo la Madaktari bingwa wa Magonjwa ya akina mama na uzazi akiwemo Dkt. Joseph Kiani pamoja na Daktari Abdallah Mashombo wakishirikiana na Madaktari bingwa wa Upasuaji wakiongozwa na Dkt. Hamis Mbarouk pamoja na timu ya wataalamu wa dawa za usingizi wakiongozwa na Dkt. Husssein Msuma
Upasuaji huo uliodumu kwa zaidi ya saa3 ulifanikiwa kuondoa uvimbe wenye uzito wa kilogramu 15 uliokuwa kwenye kizazi upande wa nje ambao ulimsumbua mwanamke huyo kwa zaidi ya miaka kumi na tano
Akizungumza mara baada ya kufanyiwa upasuaji huo mgonjwa ambaye jina lake limehifadhiwa amesema ni miaka mitano imepita tangu alipogundua ana tatizo hilo tumboni licha ya kuwa nalo kwa zaidi ya miaka 15 pasipo kujua, amewashukuru madaktari na wauguzi hospitali ya Temeke kwa huduma aliyopatiwa na mazingira mazuri ya huduma kwani hakufikiri kama tatizo hilo lingeweza kupona katika Hosptali ya Temeke
Kwa upande wake Daktari bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi ambaye alishiriki katika upasuaji wa kuondoa uvimbe huo Dkt. Joseph Kiani amesema tafiti zinaonyesha idadi kubwa ya wanawake wanaokumbana na changamoto ya vimbe hizo ni wale ambao wako katika umri wa kuzaa lakini hawajafanikiwa, au wale ambao wamepishanisha Watoto kwa miaka mingi pasipo kupata mtoto tena
Upasuaji huu wa Kibigwa ni matokeo ya uwekezaji mkubwa ambao serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Afya imeufanya wa kuhakikisha vifaa vinapatikana na wataalamu wanakuwepo ili kuwahudumia wananchi na kuokoa maisha.