TEMEKE HOSPITALI YATUMIA MAPATO YAKE KUNUNUA GARI KWAAJILI YA WATUMISHI WA HOSPITALI

Posted on: October 23rd, 2024



Menejimenti na Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke leo wakiwa na furaha wamepokea gari maalumu aina ya basi lililonunuliwa kwa mapato ya ndani ya Hospitali litakalotumika kwa shughuli mbalimbali za Hospitali na za kijamii zinazohusiana na Hospitali ikiwemo kusafirisha watumishi wanapokuwa katika majukumu ya Hospitali

Akizungumza katika hafla fupi ya kupokea gari hilo Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke Dkt. Joseph Kimaro amesema kununuliwa kwa gari hilo ni kazi iliyofanywa na kila mtumishi katika Hospitali wote wameshiriki kwa namna wanavyofanya kazi kuhakikisha Hospitali imefanikisha mpango huo kupitia mapato yake


Amesema kupatikana kwa gari hilo iwe kichocheo kwa watumishi mmoja mmoja kwamba kila jambo linawezekana na hiyo ikaongeze kasi kwa watumishi kuhakikisha kila mmoja anaendelea kuwajibika kwa manufaa na maendeleo ya Hospitali na kutimiza adhma ya serikali ya kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma bora kutoka kwa watumishi


Kwa upande wake Muuguzi Mfawidhi Hospitali ya Temeke Bi. Nuswe Ambokile amesema awali kulikuwa na changamoto nyingi zilizosababishwa na ukosefu wa usafiri ambapo Hospitali ilikuwa ikiingia gharama za zaida pale unapohitajika usafiri wa basi ikiwemo kunapotokea matukio mbalimbali kama misiba na outreach za madaktari hivyo uwepo wa gari hilo utasaidia sana utendaji kazi wa Hospitali na kuhakikisha kila mtumishi anawajibika kwa wakati katika kutoa huduma pasipokuwa na kikwazo chochote

Hafla hiyo fupi ya kupokea gari hilo imefanyika katika viunga vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke na kuhudhuriwa na watumishi na wafanyakazi wa Hospitali ya Temeke.


TEMEKE HOSPITALI YATUMIA MAPATO YAKE KUNUNUA GARI KWAAJILI YA WATUMISHI