TEMEKE HOSPITALI YAFANYA UPASUAJI WA KUTOA SARATANI YA FIGO BILA KUONDOA FIGO

Posted on: August 23rd, 2023

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke, upasuaji wa kutoa saratani ya figo bila kuondoa figo nzima umefanyika kitaalamu, upasuaji unaoitwa Nephron Sparing Nephrectomy. Upasuaji huo umefanywa na Daktari bingwa wa upasuaji wa jumla na mfumo wa mkojo, Dkt. Hussein Msuma na Daktari Msaidizi Dkt. Hamis Mbarouk.

Upasuaji huo wa kuvunja rekodi katika hospitali hiyo umeenda vizuri bila changamoto yoyote. Wiki moja iliopita Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke ilifanikiwa kufanya upasuaji wa kutoa jiwe kwenye Figo ambao pia ni upasuaji wa kwanza kufanyika hospitalini hapo. Kufanyika kwa huduma hizo inaonyesha mapinduzi Chanya ya huduma za afya zinazoendelea kutolewa Hospitalini hapo

Aidha, hospitali inaendelea kuboresha utoaji wa huduma kwa kuhakikisha huduma zote za kibingwa na kibingwa bobezi zinapatikana katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke.