TEMEKE HOSPITALI (TRRH) YAKUSANYA UNIT 365 ZA DAMU

Posted on: August 11th, 2023

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke imefanikiwa kufikia lengo la ukusanyaji damu kwa kupata unit 365 za damu leo katika zoezi la uchangishaji damu lililoandaliwa na hospitali hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya JAI. 

Mkurugenzi wa Hospitali Dkt. Joseph Kimaro ameendelea kutoa wito kwa jamii kujitokeza kwa wingi zaidi kuchangia Damu kwa siku ya kesho tarehe 13/08/2023 katika viwanja vya DUCE.