PSSSF YAIPA TUZO MAALUMU HOSPITALI YA TEMEKE KWA KUWA MFANO WA KUIGWA WA KUWASILISHA MICHANGO YA WATUMISHI KWA WAKATI
Posted on: October 20th, 2025Tuzo hiyo maalumu imetolewa tarehe 10.10.2025 na bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF ambayo imelenga kutambua mchango wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Temeke katika kupeleka michango ya watumishi wake PSSSF kwa wakati lakini pia utoaji wa huduma bora na kwa kuonyesha ushirikiano wa kuigwa kwa mfuko wa PSSSF
Tuzo hiyo imepokelewa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Temeke Dkt. Joseph Kimaro akiambatana na viongozi wengine wa Hospitali katika shughuli maalumu ya kuadhimisha kilele cha Wiki ya huduma kwa wateja zilizofanyika Ofisi za PSSSF Temeke






