Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke, Dkt Joseph Kimaro amchangisha Damu Mkuu wa wilaya ya Temeke, Mhe. Sixtus Mapunda katika ofisi za Toyota Tanzania

Posted on: November 6th, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sixtus Mapunda amewataka wananchi kuwa na utaratibu wa kuchangia damu wanapopata wasaa kwani ni kitendo cha kishujaa chenye lengo la kuokoa maisha ya wengine.

Ameyasema hayo wakati akifunga zoezi hilo na kusema kuwa kutoa damu ni jambo zuri, leo nitachangia damu kwaajili ya kusaidia wengine na kuwa balozi mzuri katika kuhamashisha wananchi katika zoezi la uchangiaji damu unaokuwa endelevu.

“Kila anaechangisha damu ni shujaa, kwa sababu ni mtu ambae yupo tayari kujitoa kwaajili ya mwingine pia kila unit moja inayopatikana inasaidia kwa kiasi kikubwa kuokoa maisha ya watu”. Amesema Mhe. Mapunda

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke Dkt Joseph Kimaro amewashukuru wafanyakazi wa Toyota ambao kwa wamejitoa na kuweza kuchangia damu ambayo itaenda kuwasaidia wagonjwa wenye uhitaji.

“Uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara ya Afya katika hospitali ya rufaa ya mkoa Temeke kwa kuwa na vifaa vya kisasa vya kiuchunguzi kama vile CT scan za kisasa na x-ray za kidigitali, ukarabati wa jengo la huduma za dharula (EMD) na kuweza kununua mashine za kuweza kuendesha maisha (Ventilators) hivyo kuboresha utoaji huduma katika hospitali hiyo” amesema Dkt. Kimaro

Kwa hatua nyingine, Dkt. Kimaro aliweza kumtoa damu Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sixtus Mapunda kwa ajili ya zoezi la kuchangia damu ambalo llililokuwa likiendeshwa kwa siku tano