GARI MAALUMU KWA AJILI YA MAMA NA MTOTO SASA LINAPATIKANA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA TEMEKE

Posted on: August 25th, 2024

Dar es salaam, 27 Agosti 2024


Katika kuhakikisha vifo vya mama na mtoto vinapungua hasa vinavyosababishwa na wagonjwa kuchelewa kufika Hospitali, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke kwa kutambua changamoto hiyo imeleta gari la wagonjwa (Ambulance) maalumu kwaajili ya mama na mtoto linalotumika kumfuata mama au mtoto anapopata tatizo ili kumuwaisha Hospitali hapo

Akizungumza katika mahojiano aliyoyafanya na TBC, Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke Dkt Joseph Kimaro amesema katika mpango wa fedha wa mwaka 2024/2025 Hospitali ya Mkoa ya Temeke imejipanga kuendelea kutoa huduma bora na za kibingwa kwa watoto ili kupunguza vifo vya mama na watoto ambapo mpaka sasa tayari imeanzishwa Neonatal ICU level 2 ili kuendelea kutoa huduma za ICU kwa watoto Hospitali hapo


Gari hilo maalumu kwa mama na mtoto limekuwa na mafanikio makubwa kwasababu limeweza kusaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto ambavyo husababishwa na kuchelewa kufika Hospitali kupata huduma ambapo kwasasa huweza kupita miezi miwili hakujatokea kifo cha mama wala mtoto  vinavyosababishwa na  kuchelewa Hospitali kwa kukosa usafiri.