Dental( kinywa na Meno)

Posted on: July 12th, 2024

Idara ya Kinywa na Meno

Karibu Idara ya Kinywa na Meno katika Hospital ya Rufaa ya Mkoa Temeke tunajivunia kutoa huduma bora za afya ya kinywa na meno kwa jamii inayotuzunguka, pamoja na wageni kutoka sehemu mbalimbali nchini. Tunajikita katika kutoa elimu na ushauri wa kina kuhusu afya ya kinywa na meno, kwa lengo la kudumisha afya njema na kuzuia matatizo ya kinywa na meno.

*Huduma Zinazotolewa:*
1. Elimu na ushauri wa Afya ya Kinywa na Meno
2. Kung’oa Meno
3. Kuziba Meno
4. Kusafisha na Kung’arisha Meno
5. Kutengeneza Meno Bandia ya Kuvua na Kutovua
6. Upasuaji wa Kinywa na Meno
7. Kurudishia Taya Zilizovunjika
8. Kurekebisha Taya na Kupanga Meno
9. Kutengeneza Vifaa vya Kuvaa na Kuvua kwa Ajili ya Kupanga Meno
10. Kuziba Meno Kuanzia Kwenye Mizizi

Idara yetu inahudumia kati ya wagonjwa 140 hadi 200 kila mwezi. Tumeboresha huduma zetu kwa kupokea mashine ya Periapical Dental Xray.

*kwanini uje kwetu?:*
- Tunajivunia kutoa huduma bora na ya kibingwa kwa wagonjwa wetu, hususan katika kurekebisha mpangilio wa meno na taya (Orthodontic), huku tukitoa fursa kwa wagonjwa kulipia kwa fedha taslimu au kupitia bima zao.
- Tumeeneza ufikiaji wa huduma zetu katika vyuo, shule za sekondari, na hospitali za wilaya kupitia programu yetu ya Mkoba.
- Kila siku za kazi, tunahakikisha tunatoa matibabu ya kinywa na meno kwa ufanisi na kwa uangalifu wa hali ya juu.

Tunaahidi kuendelea kutoa huduma bora, kuboresha ufikiaji wa matibabu, na kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha afya bora ya kinywa na meno kwa jamii yetu. Karibu katika Idara yetu ya Kinywa na Meno, ambapo afya yako ya kinywa ni jukumu letu