WATUMISHI HOSPITALI YA TEMEKE WAJENGEWA UWEZO UTUNZAJI WA NYARAKA ZA SERIKALI
Posted on: November 3rd, 2024Dar es salaam 4 Novemba, 2024
Menejimenti na baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Rufaaa ya Mkoa Temeke leo wamepokea mafuzo maalumu ya namna bora ya kutunza na kuhifadhi nyaraka mbalimbali za serikali kwa usalama ili zitumike kama zilizopangwa na kwa kipindi husika
Mafunzo hayo yameeendeshwa na Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw Firimin Msiangi ambapo mafunzo hayo yamejikita kuwapa elimu watumishi juu ya namna bora ya kutunza nyaraka mbalimbali za serikali kwa usiri kama ambavyo zimekusudiwa
Aidha watumishi wamekumbushwa kuendelea kutanguliza mbele uzalendo na kuzingatia maadili ya taaluma zao wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ikiwemo kuwa na namna bora ya kutunza nyaraka za serikali ili ziweze kuhifadhiwa na kutumika kama ilivyopangwa na serikali ambapo pia watumishi wamekumbushwa kuzingatia sera ya taifa ya kumbukumbu na nyaraka ya mwaka 2011 inayosisitiza taasisi za serikali kuhakikisha zinatunza nyaraka zake kwa matumizi ya taasisi na taifa kwa ujumla
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke, Dkt. Joseph Kimaro ameshukuru kwa watumishi kupewa elimu hiyo iliyolenga kuwajengea uwezo watumishi wa kutunza nyaraka za serikali ambapo amesema watumishi Hospitali ya Temeke watazingatia miongozo yote ambayo inatolewa na serikali ili kuboresha utendaji kazi na kuhakikisha nyaraka za serikali zinatunzwa katika njia nzuri na salama kwa matumizi ya baadae