WANAFUNZI WA UDAKTARI 20 KUTOKA SUDAN KUJIUNGA NA TIMU YA AFYA YA TEMEKE HOSPITALI KWA AJILI YA MAFUNZO

Posted on: January 1st, 2024

WANAFUNZI WA UDAKTARI 20 KUTOKA SUDAN KUJIUNGA NA TIMU YA AFYA YA TEMEKE HOSPITALI KWA AJILI YA MAFUNZO

Dar es Salaam, Tarehe 01/01/2024

Wanafunzi 20 wa udaktari kutoka chuo kikuu cha Tiba, Sayansi na Teknolojia (UMST) cha Khartoum nchini sudani wanatarajia kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke(TRRH) kama moja ya hatua ya kuongeza ujuzi katika fani ya udaktari baada ya kukamilisha kipindi chao cha mafunzo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

Uhamisho huo kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbi (MNH) na kuelekea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke(TRRH) unatarajia kufanyika kuanzia tarehe 02 Januari 2024 kwa kuzingatia lengo la kuwawezesha kupanua ujuzi wao na kujifunza mazingira tofauti ya utunzaji wa afya.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke, Dkt. Joseph Kimaro,amesema, “Tunafurahi kuwakaribisha wanafunzi hawa wa UMST katika timu yetu ya wataalamu wa afya kwani tupo tayari kutoa ushirikiano kwa wanafunzi na kuhakikisha wanapata elimu bora na mafunzo sahihi yatakayowawezesha kuwa madaktari wenye ujuzi” ameyasema hayo mara baada ya mazungumzo makini kati uongozi wa TRRH, na Profesa Mamoun Homeida kutoka Chuo cha Tiba, Sayansi na Teknolojia (UMST).

Wanafunzi hawa wanatarajia  kujiunga na idara mbalimbali za hospitali hiyo, kama vile idara ya mifupa, watoto, Upasuaji, Upasuaji njia ya Mkojo, magonjwa ya ndani, na idara ya wanawake na uzazi. Kila idara inawakilisha fursa kwa wanafunzi hawa kuendeleza stadi zao na kujenga misingi imara ya ujuzi wa udaktari.