USHIRIKA AFYA NI MKOMBOZI WA AFYA YA MKULIMA- WAZIRI UMMY
Posted on: September 19th, 2019WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa mpango wa Ushirika Afya ndio njia pekee na ya kisasa inayomwezesha mkulima kuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wowote na kuepukana na upotevu wa fedha nyingi kwa kulipia gharama za matibabu.