TEMEKE HOSPITALI YAKUSANYA UNIT 290 KATIKA MASHINDANO YA POLISI JAMII CUP*

Posted on: September 23rd, 2023

TEMEKE HOSPITALI YAKUSANYA UNIT 290 KATIKA MASHINDANO YA POLISI JAMII CUPTemeke, Dar es Salaam,
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke imeshiriki Mashindano ya Polisi Jamii Cup ambayo yamekuwa yakifanyika kuanzia tarehe 4 hadi tarehe 24 Septemba. Mashindano hayo yamekuwa yakilenga kuimarisha mahusiano kati ya jeshi la polisi na jamii. Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke imeweza kutoa vifaa tiba na kufanikisha zoezi la uchangiaji damu kwa wanafunzi wa Chuo cha Polisi(DPA) na wakazi wa eneo la Temeke waliojitokeza.

Mchango muhimu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke katika mashindano haya umegusa maisha ya watu na jamii nzima kwani Hospitali hii imefanikiwa kukusanya jumla ya unit 290 za damu, jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza akiba ya damu inayohitajika katika huduma za matibabu.

Akizungumza katika kuhitimisha mashindano hayo, Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke, Dr. Joseph Kimaro, ameshukuru sana uongozi wa Chuo cha Polisi Dar es Salaam (DPA) kwa kuleta pamoja wizara mbili muhimu, Wizara ya Afya na Wizara ya Ulinzi, katika kuleta maendeleo ya taifa. Amesisitiza kuwa michezo kama hii ina jukumu kubwa katika kujenga mazingira rafiki kati ya jeshi la polisi na jamii.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi, SACP Mambosasa ambae pia ni Mkuu wa Chuo cha Polisi Dar es salaam(DPA) amesema kuwa, kupitia michezo kama hii itasaidia kuokoa vijana wetu katika wimbi la kujihusihsa na uhalifu hasa wa madawa ya kulevya na vilevile kufungua fursa zitokanazo na michezo.

Aidha, SACP Mambosasa amesema kuwa kupitia michezo hii wanaokoa maisha ya watu wanao hudumiwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa Temeke, kwani  mashindano haya yameamabatana na uchangiaji damu wa hiari kwa lengo la kujenga uwezo katika benki ya damu salama na kuendelea kuokoa wahanga wa ajali, kina mama wanao jifungua na wagonjwa wengine