MSD YAIPONGEZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA TEMEKE KWA KUANZISHA HUDUMA ZA DIALYSIS

Posted on: August 27th, 2024

Dar es salaam, 27 Agosti 2024 


Pongezi hizo zimetolewa na muwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa MSD ndugu Betia katika hafla fupi ya kuishukuru MSD kwa mchango wao mkubwa katika kuboresha huduma za Afya Hospitalini hapo

Ndugu Betia amesema MSD imejipanga kuhakikisha huduma inayotolewa Hospitali ya Temeke itakuwa endelevu na haitoweza kusitishwa kwasababu ya ukosefu wa huduma au vifaa na itaendelea kuhakikisha kila huduma, dawa au kifaa kinachohitajika kinapatikana kwa wakati

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Temeke Dkt Joseph Kimaro amesema kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Hospitali ya Temeke imekuwa ikishirikiana na Bohari ya Dawa nchini (MSD) ushirikiano ulioiwezesha Hospitali ya Temeke kuboresha huduma zake hasa matibabu na usafishaji wa Figo ambapo kwa kushirikiana wameweza kufunga mashine maalumu na huduma za usafishaji figo tayari zinatolewa Hospitali ambapo mpaka sasa wagonjwa wanaendelea kupatiwa huduma

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Temeke pia imetoa tuzo ya pongezi kwa kutambua mchango wa Bohari ya dawa Nchini katika kuboresha huduma za Afya katika hospitali ya Temeke ikiwemo kuwezesha huduma za usafishaji figo kufanyika kikamilifu.