MGANGA MFAWIDHI HOSPITALI YA TEMEKE AWAHIMIZA WATUMISHI KUTIMIZA WAJIBU WAO KIKAMILIFU

Posted on: September 23rd, 2024

Dar es Salaam, 26 Septemba, 2024


Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke Dkt. Joseph Kimaro amezungumza na watumishi wa Hospitali kutoka vitengo vyote ikiwa ni sehemu ya kutoa mrejesho wa yaliyojadiliwa kwenye mkutano wa waganga wafawidhi wa Hospitali za Rufaa kilichofanyika mwezi huu mkoani Mbeya

Dkt Kimaro amewataka watumishi wote kuhakikisha kila mmoja anatambua kwamba ubora wa huduma za Hospitali unatokana na kila mmoja kuwajibika kwa nafasi yake kikamilifu


Amesema kila mtu akitimiza wajibu wake na nafasi yake malengo ya serikali na wizara ya afya ya kuwasaidia wananchi yatatimia kwa kiwango kikubwa

"Zipo idara ambazo zimefanya vizuri na tunajivunia kama Hospitali ikiwemo idara ya famasia ambapo kwasasa tunauhakika wa dawa kwa zaidi ya asilimia 90, idara ya Radiolojia, Upasuaji na nyingne lakini pia zipo idara ambazo mwenendo wake bado hauridhishi, naendelea kuwakimbusha kila mmoja ajue wajibu wake na autekeleze kikamilifu"



Aidha Dkt Kimaro amesema yapo mengi mazuri yanayofanywa na Hospitali lakini hayawafikii wananchi moja kwa moja ambapo amesisitiza mambo yote makubwa yanayofanyika ndani ya Hospitali kuhakikisha yanawafikia wananchi kwa kushirikiana na kitengo cha Uhusiano kwa umma ili wananchi waone namna ambavyo serikali inaboresha huduma kwa manufaa ya wananchi wake

"Zipo kesi nyingi tunazipokea kama wataalamu wa afya, wapo wagonjwa wanaokuja kufanyiwa upasuaji wa matatizo ambayo kwa mazingira yetu ni mageni na zamani wengi walikuwa wanaenda kutibiwa nje lakini kwasasa huduma zote zinafanyika hapa na wagonjwa wanapona"



Dkt. Kimaro amezitaka kila idara za Hospitali kuendelea kujipanga na kujiimarisha zaidi katika kutoa huduma bora ili kuhakikisha wananchi wanaofika Temeke kupata huduma wanaridhiswa na huduma zinazotolewa