Hospitali ya Temeke yaanza kutoa chanjo ya UVIKO-19
Posted on: August 3rd, 2021Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke yaanza rasmi zoezi la utoaji wa chanjo ya UVIKO-19 kwa watu wenye vigezo. Vigezo vya kupata chanjo ni pamoja na:
1. Awe na Umri kuanzia miaka 50 na kuendelea
2. Watumishi wa sekta ya afya (umri wowote)
3. Wenye matatizo ya kiafya pamoja na magonjwa sugu kama kisukari
4. Awe amekubali kuchanja kwa hiari yake mwenyew
Fika na kitambulisho cha NIDA,Hati ya kusafiria au leseni ya udereva au kitambulisho kinachotambuliwa kisheria
Pichani ni Mkurugenzi wa Hospitali Dr. Meshack Shimwela MD akichanjwa chanjo ya UVIKO-19