DKT JINGU AKOSHWA NA HUDUMA ZA DIALYSIS ZINAVYOTOLEWA KWA BEI NAFUU HOSPITALI YA TEMEKE

Posted on: August 28th, 2024

Dar es salaam 28 Agosti, 2024


Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt.John Jingu , ameyasema hayo Agosti 26, 2024 katika ziara yake ya kikazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Temeke , ambapo amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo jengo la kutolea huduma za Usafishaji damu (Dialysis) na kujionea shughuli za utoaji huduma zinavyotolewa Hospitali hapo.


Katika ziara hiyo Katibu Mkuu  Dkt John Jingu amezungumza na uongozi na watumishi wa Hospitali ya Temeke ambapo amepongeza namna huduma zinavyotolewa hasa za usafishaji damu (Dialysis) ambazo zinatolewa kwa bei nafuu hali inayowezesha wananchi kupata huduma hiyo kwa unafuu kulingana na hali zao.


Aidha Katibu Mkuu amewataka watumishi wote wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Temeke na watumishi wa wizara ya Afya kuhakikisha wanaendelea kulinda na kuheshimu maadili ya taaluma ya udaktari pamoja na maadili ya utumishi wa umma katika kutoa huduma kwa wananchi, pia amesisitiza utoaji wa huduma kwa wananchi (wagonjwa) uwe wa uharaka na kuboresha mawasiliano na wagonjwa panapokua na changamoto .


Dkt Jingu amesisitiza  matumizi ya lugha rafiki kwa wagonjwa katika kutoa huduma ili wananchi katika Hospitali za serikali,

 pia ameipongeza Hospitali ya Temeke kwa kuendelea kutoa huduma za mkoba kwa wananchi


Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke Dkt Joseph Kimaro amesema ujio wa Katibu Mkuu katika Hospitali ya Temeke ni jambo la msingi kwasababu imesaidia kujua kiwango cha ubora wa huduma zinazotolewa na amesema changamoto mbalimbali zilizojitokeza zitaendelea kutatuliwa ili kuhakikisha wananchi wa Temeke na maeneo mengine wanaofika Hospitali hapo wanapata huduma bora


Hata hivyo, katika ziara hiyo Katibu Mkuu Dkt John Jingu ametembelea maeneo mbalimbali ikiwemo sehemu ya mapokezi ya wagonjwa wa nje (OPD), jengo la huduma za mionzi (Radiology) pia amezungumza na baadhi ya wagonjwa waliofika kupata matibabu ikiwa ni sehemu ya kuboresha huduma kwa wananchi.