Laboratory

HUDUMA ZA MAABARA:

Maabara ni kitengo  cha uchunguzi wa Afya ya binadamu,hivyo ni sehemu muhimu kwa daktari katika kufanya maamuzi katika kumtibu mgonjwa,lakini pia Maabara inatumika kufanya uchunguzi ili kuweza kuratibu vyema shughuli za Kinga.Hivyo,Maabara ni sehemu muhimu katika uendeshaji wa hospitali.

Maabara ya Hospitali ya Rufaa Mkoa Temeke ina wataalam 16 waliosajiliwa.

Ngazi ya Shahada wapo wataalam 4 na ngazi ya Stashahada ni wataalam 12.

Lakini pia ina Mhudumu mmoja.


Maabara ya Hospitali ya Rufaa Temeke inaongozwa na Mtaalam Kiongozi

Venance Martin Mlowe (Afisa Mteknolojia) -BMLS

Idara ya Maabara imegawanyika katika vitengo saba (7) ambavyo ni:

-Mapokezi & Phlebotomy

-Hematology

-Microbiology

-Parasitology

-Clinical Chemistry

-Serology

-Blood donation na Blood Transfusion

Idara ya Maabara kupitia vitengo hivyo,ina majukumu ya kupima afya  za binadamu kwa lengo la kurahisisha matibabu kwa wagonjwa,lakini pia kwa lengo la kuweza kutoa kinga kwa wananchi kabla ya kupata magonjwa.

Wateja wetu  ni wagonjwa waliolazwa mawodini au wagonjwa toka nyumbani.

Tunapokea wateja wanaohudumiwa kwa Bima za Afya kama NHIF, NSSF na CHF.

Maabara hii pia inatumika kama Maabara ya kufundishia,ambapo tunapokea wanafunzi toka vyuo vya Maabara za Afya vilivyosajiliwa na TCU au NACTE kwa ajili ya kufanya mazoezi kwa vitendo ili kupata ujuzi.Pia tunapokea wataalam wa Maabara baada ya kumaliza shahada ya kwanza ili waweze kufanya mafuzo tarajali (internship kwa muda wa Mwaka mmoja kabla ya kuomba usajili wa kudumu katika baraza la la wataalam Maabara-Tanzania.


Karibu Maabara ya Temeke uapte hudumu inayozingatia miongozo ya ubora wa Kimataifa (ISO15189:2012)