TAARIFA YA KIFO CHA MFANYAKAZI WA TEMEKE HOSPITALI DKT. BARAKA ABDALLAH HOKI
Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke Dkt Joseph Kimaro anasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi Dkt. Baraka Abdallah Hoki aliyekuwa akihudumu katika idara ya mifupa katika Hospitali ya Temeke kilichotokea katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali alipokuwa akitoka kazini
Menejimenti na uongozi wa Hospitali unatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na wafanykazi wenzake marehemu kwa msiba huu mzito
Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe